Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

Wakaazi wa Gao kaskazini mwa Mali waandamana dhidi ya waasi

 Wakaazi wa mji wa Gao wa kaskazini mwa Mali wamefanya maandamano kulaani hatua ya waasi wa Tuareg ya kuukaliwa kwa mabavu mji wao huo.
Mamia ya wananchi wa mji huo wanalalamikia kuvamiwa mji huo na waasi hao wa Tuareg pamoja na makundi mengine ya waasi, kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Machi nchini Mali.
Waandamanaji wamechoma moto matairi ya gari huku makundi ya waasi yanayodhibiti mji huo yakifyatua risasi hewani kujaribu kuwatawanya waandamanaji. Watu wasiopungua watano wamejeruhiwa katika maandamano hayo.
Makundi ya waasi ya kaskazini mwa Mali yanayodaiwa kuwa na mfungamano na mtandao wa al Qaida, hivi sasa yanalidhibiti eneo lote la kaskazini mwa Mali.

No comments: