Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 3, 2012

Maoni: Marekani imemrubuni Rais Hamid Karzai wa Afghanistan

Siku moja baada ya Rais Hamid Karzai wa Afghanistan kukubali wanajeshi wa Marekani wabakie nchini mwake hadi 2024, maoni mbalimbali yametolewa kuhusiana na hatua hiyo. Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la kila siku la The Afghan Daily umebaini kuwa Waafghani wengi hawakubaliani na uamuzi huo wa Rais Karzai. Baadhi ya wachambuzi wameliambia gazeti hilo kuwa Rais Barack Obama wa Marekani amemrubuni Rais Karzai kusaini makubaliano hayo hapo jana mjini Kabul. Rais Obama ambaye alifanya ziara ya kushtukiza huko Afghanistan usiku wa kuamkia leo, amesema kuwa Kabul na Washington zimekubali kushirikiana katika masuala mbalimbali likiwemo suala muhimu la Usalama. Weledi wa mambo wanasema kuingia kinyemela Rais Obama huko Afghanistan tena usiku wa manane ni ishara ya jinsi Marekani ilivyopoteza itibari na uungwaji mkono nchini humo.

No comments: