Uchaguzi wa Bunge wa Angola unatarajiwa kufanyika Agosti 31 mwaka huu. Kuna uwezekano mkubwa kwa Rais Jose Eduardo dos Santos kuendelea kuongoza nchini hiyo.
Dos Santos anaongoza nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa miaka 32 sasa.
Ofisi ya Rais Dos Santos ilitangaza jana kwamba uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Baraza la Taifa, ambayo ni bodi ya ushauri yenye wajumbe 19 wakiwemo maafisa wa ngazi za juu wa serikali, viongozi wa upinzani na majaji kadhaa wa mahakama.
Uchaguzi huo utakuwa ni wa pili kufanyika katika nchi hiyo ya pili kwa kuzalisha mafuta kwa wingi barani Afrika, tangu vilipomalizika vita vya miaka 27 vya wenyewe kwa wenyewe, mwaka 2002.
Baada ya chama cha MPLA cha Rais Dos Santos kuwashinda waasi wa UNITA, kilichuana na wapinzani wake katika uchaguzi wa mwaka 2008 na kupata ushindi wa asilimia 82 ya kura.
Hivi sasa Dos Santos anahesabiwa kuwa ni mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika baada ya yule wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

No comments:
Post a Comment