Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 23, 2012

Ahmadinejad asisitiza kuhusu kuimarishwa uhusiano wa Iran na Kenya

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na balozi wa Kenya nchini Iran na kusisitiza kuhusu udharura wa kuimarishwa na kuinuliwa kiwango cha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Ikulu ya Rais mjini Tehran, Rais Ahmadinejad pia ameashiria uhusiano mzuri baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya.
Aidha katika mkutano huo, Balozi wa Kenya nchini Iran Dkt. Rashid Ali amemkabidhi rais Ahmadinejad ujumbe kutoka kwa Rais Mwaki Kibaki wa Kenya.

No comments: