Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 3, 2012

Kiongozi Muadhamu: Taifa la Iran linamfahamu vyema adui yake

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siku ya Ijumaa tarehe 4 Mei , kwa mara nyingine taifa la Iran litaonyesha muono wa mbali na kuijua vizuri hali na mazingira yanayotawala. Kiongozi Muadhamu Ayatullah Khamenei ameyasema hayo hii leo alipokutana na maelfu ya walimu kutoka maeneo mbali mbali ya Iran hapa mjini Tehran. Akiashiria awamu ya pili ya uchaguzi wa tisa wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran, Ayatullah Khamenei amesema, siku ya Ijumaa wananchi wa Iran wataonyesha muono wao wa mbali na jinsi wanavyoijua vizuri hali na mazingira wanayoishi kwa kuhudhuria kwa wingi katika vituo vya kupigia kura. Amesema, taifa la Iran kwa kutegemea welewa wake mkubwa, liliweza kuonyesha umakini wake wa hali ya juu kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa awamu ya kwanza ya uchaguzi wa tisa wa Majlisi ya Kiislamu uliofanyika tarehe 2 mwezi Machi mwaka huu. Aidha amesema, kwa kuzingatia hali ya inayotawala duniani hivi sasa, ambapo mataifa yote ili kufikia mafanikio yanapaswa kuingia katika medani mbalimbali kwa mwamko na welewa wa hali ya juu na kuongeza kuwa, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu wananchi wa Iran hawako nyuma katika jambo hilo na kwamba, taifa hili linamfahamu vyema adui yake na halidanganyiki na madai ya adui ya kujifanya kuwa ni rafiki wa taifa la Iran.

No comments: