Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yameendelea kufanya mashambulio dhidi ya waasi wenye ngome zao mashariki mwa nchi hiyo. Msemaji wa Jeshi la Congo ameziambia duru za habari kwamba, jeshi la nchi hiyo limeendelea kufanya mashambulio yake mashariki mwa nchi hiyo likizilenga ngome za waasi hao. Taarifa ya jeshi la Congo inasema kuwa, hivi sasa jeshi hilo limo katika kuwarejesha nyuma waasi hao. Wakati huo huo, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuwa, linadhibiti hali ya mambo mashariki mwa Congo hasa huko Kivu Kaskazini. Huku hayo yakiripotiwa, maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameendelea kukimbilia katika nchi jirani za Rwanda na Uganda wakikimbia machafuko mapya yaliyobuka mashariki mwa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment