Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, April 27, 2012

Wizara ya Fedha ya Tanzania yaahidi ubadhirifu wa mikataba mibovu kutotokea tena

Wizara ya Fedha ya Tanzania imesema baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali kubaini matumizi mabovu ya mishahara hewa na mikataba mibovu, wizara hiyo haitarajii kujitokeza tena kwa ubadhirifu huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Mohamed Mtonga wakati akifufunga semina ya siku nne ya maodita wa ndani jijini Dar es Salaam. Alisema lengo la semina kwa washiriki hao ni kuwajengea uwezo ambao utawasaidia katika kazi zao hasa kudundua maeneo hatarishi ya upotevu wa fedha. Mtonga amebainisha kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kubaini matumizi yasiyo ya kawaida kwa haraka kwa kuwa wizara imeanzisha mfumo mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya kompyuta. Amesema teknolojia hiyo ya kisasa ambayo ina uwezo wa kugundua makosa hayo haraka katika maeneo mbalimbali, hivi sasa inatumika katika nchi ya Kenya ambapo imefanikiwa kwa kiwango cha juu. Aidha, amesema Wizara ya Fedha imetoa muongozo unaowataka kila Katibu Mkuu wa Wizara kufanya uchunguzi katika kubaini maeneo hatarishi katika ofisi zao kitendo kitakachowasaidia kugundua haraka ubadhirifu wa mishahara hewa na mikataba bandia kwa kutumia teknolojia hiyo.../

No comments: