Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, April 27, 2012

Usalama waimarishwa nchini Nigeria baada ya kutokea mashambulio ya kigaidi

Vyombo vya usalama nchini Nigeria vimeimarisha usalama kuanzia Ijumaa ya leo kufuatia milipuko iliyotokea jana katika ofisi za gazeti mashuhuri nchini humo. Sambamba na kushadidisha usalama mjini Abuja, vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimeanza uchunguzi kuhusiana na mashambulio hayo ya kigaidi ambayo hayajawahi kushuhudiwa. Watu wasiopungua tisa walifariki dunia hapo jana baada ya ofisi za gazeti lenye wasomaji wengi la This Day mjini Abuja na Kaduna kushambuliwa.
Msemaji wa Polisi ya Abuja ameashiria mashambulio hayo ya jana na kubainisha kwamba, usalama umemairishwa zaidi tangu hiyo jana hasa katika maeneo ya kando kando na ofisi za vyombo vya habari. Aidha hatua za usalama zimeimarishwa pia katika mji mkuu wa kiuchumi wa Nigeria wa Lagos. Kundi lenye kufurutu ada la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulio ya kigaidi nchini humo, kama njia ya kuishinikiza serikali ya Abuja kuwaachilia huru wanachama wake waliokamatwa.

No comments: