Mlipuko mkubwa umejiri katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo watu 10 wameuawa wakiwemo Mkuu wa Kamati ya Olimpiki na Mkuu Shirikisho la Soka Somalia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Radio Tehran, watu wengine wengi wamejeruhiwa wakati mwanamke gaidi aliyekuwa amesheheni bomu alipojirupua ndani ya Jumba la Kitaifa la Tamthilia Mogadishu Jumatano mchana.
Hujuma hiyo ya kigaidi imejiri katika hafla ya kuadhimisha mwaka moja tokea ianzishwe Televisheni ya Kitaifa ya Somalia. Maafisa wa ngazi za juu wa Somalia akiwemo Waziri Mkuu Abdiweli Mohammad Ali na mawaziri saba walikuwa ndani ya jengo hilo. Imearifiwa kuwa waziri mkuu huyo amenusurika bila kujeruhiwa. Polisi Somalia wamethibitisha kuuawa Mkuu wa Shirikisho la Soka Somalia Said Mohammad Nur na Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Somalia Aden Yabarow Wish. Kundi lenye misimamo mikali la al Shabab limedai kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment