Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, April 27, 2012

Rais Joyce Banda wa Malawi atangaza baraza jipya la mawaziri


Rais Mpya wa Malawi Bi Joyce Banda ametangaza baraza lake jipya la mawaziri ambapo amewachagua shakhsiya kutoka vyama kadhaa vya upinzani katika juhudi za kujaribu kupata uungaji mkono mkubwa wa bunge na kuwavutia wafadhili wa kimataifa kurejea tena huko Malawi. Rais Banda wa Malawi ambaye wiki hii alimfuta kazi gavana wa benki kuu ya nchi hiyo na mapema mwezi huu kukumfukuza Waziri wa Habari wa nchi hiyo amembakisha kwenye nafasi yake Ken Lipenga Waziri wa Fedha wa Malawi. Rais Joyce Banda ambaye ni mtetezi mashuhuri wa haki za wanawake na Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo amekuwa akifanya juhudi za kuiondoa Malawi katika mgogoro wa kiuchumi baada ya kuibuka mgogoro kati ya Rais aliyemtangulia hayati Bingu wa Mutharika na wafadhili wa kimataifa.

No comments: