Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, April 25, 2012

Wanafunzi weusi wa vyuo vikuu Uingereza wanabaguliwa

Ripoti iliyotolewa huko Uingereza imethibitisha kuwa wanafunzi weusi wa vyuo vikuu nchini humo wanabaguliwa na hawapewi fursa sawa na zile wanazopewa wanafunzi wenzao wazungu.
Televisheni ya Press imeripoti kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya Tasisi ya Takwimu za Elimu ya Juu nchini Uingereza fursa za kazi za wanafunzi weusi wanaohitimu masomo nchini humo ni chini ya asilimia 30 ikilinganishwa na wenzao wazungu.
Vilevile uchunguzi wa mashirika ya Elevation Networks na Bow Group umebaini kuwa hata wale Waingereza weusi wanaohitimu masomo wanaopata nafasi za kazi hupewa mishara midogo zaidi ya ile wanayopewa wenzao wazungu.
Uchubguzi huo pia umesema kuwa asilimia 40 ya Waingereza weusi wanasumbuliwa na ubaguzi katika maeneo yao ya kazi.

No comments: