Mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kutetea haki za binadamu wameandamana na kukusanyika nje ya kanisa moja huko kusini mwa Los Angeles wakilalamikia kuongezeka vitendo vya ukandamizaji na ubaguzi wa rangi vinavyoilenga jamii ya raia Marekani wenye asili ya Afrika. Ndugu wa vijana wawili wa Kimarekani wenye asili ya Afrika waliouawa hivi karibuni na mlinzi wa Kimarekani na maafisa polisi wa nchi hiyo pia wameshiriki kwenye maandamano hayo. Maandamano hayo yamefanyika katika kukumbuka kutimia miezi miwili tangu kuuawa Trayvon Martin kijana Mmarekani mweusi aliyekuwa na umri wa miaka 17. Martin aliuawa na mlinzi mmoja mzungu kwa jina la George Zimmerman ambaye polisi ya Marekani ilimwachia huru baada ya mauaji hayo. Hata hivyo maandamano makubwa yaliyofanywa nchini Marekani mapema mwezi huu kulalamikia mauaji hayo hatimaye yalipelekea polisi ya Marekani kuagiza kutiwa mbaroni muuaji Zimmerman na kumshtaki kwa mauaji hayo. Watetezi wa haki za binadamu walioshiriki kwenye maandamano hayo kama vile wachungaji Al Sharpton na Jesse Jackson wametaka sheria ichukuye mkonodo wake na hatua kali zichukuliwe ili kuzuia vitendo vya ubaguzi wa rangi vinavyoendelea kushtadi huko Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment