Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, April 27, 2012

Waziri Mkuu wa Jordan ajiuzulu ghafla

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Waziri Mkuu wa Jordan Awn Al-Khasawneh amekabidhi barua rasmi ya kujiuzulu wadhifa wake huo kwa Mfalme Abdullah wa Pili wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa gazeti la al Quds al Arabi al Khasawneh alikabidhi barua yake hiyo jana jioni saa chache baada ya Mfalme wa Jordan kutoa amri ya kurefushwa muhula wa bunge la sasa hadi mwezi Juni. Hii ni katika hali ambayo serikali ya Waziri Mkuu al Khasawneh ilikuwa imetaka bunge likamilishe muhula wake katika muda wake wa kisheria. Duru za habari zimeripoti kuwa kumekuwepo na hitilafu kati ya Waziri Mkuu na Mfalme Abdullah wa Pili juu ya masuala yanayohusiana na uchaguzi na muhula wa kuhudumu bunge. Bila kutaja sababu ya kuchukua uamuzi huo, al Khasawneh, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Uturuki amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kupitia Waziri wa Nchi anayehusika na masuala ya sheria Ibrahim al Jazi suala linalodhihirisha hitilafu kubwa zilizopo kati ya serikali na Mfalme nchini Jordan. Ripoti zaidi zinasema Mfalme Abdullah wa Pili amekubali kujiuzulu kwa Waziri Mkuu al Khasawneh na kumteua Fayez al-Tarawneh kujaza nafasi hiyo.../

No comments: