Jumamosi ya leo harakati ya wapinzani wa serikali ya Senegal kwa mara nyingine tena ina mpango wa kuandamana dhidi ya serikali huko Dakar mji mkuu wa nchi hiyo, wakati ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kieneo ya ECOWAS ukitarajiwa kuelekea Senegal kwa lengo la kufanya upatanishi kati ya pande hizo mbili. Katika kikao chao kilichofanyika huko Nigeria, viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) wamepasisha kutuma ujumbe wa pamoja wa AU na ECOWAS huko Senegal.
Hatua ya Rais Abdullaye Wade wa Senegal mwenye umri wa miaka 85 ya
kutaka kugombea tena katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo ndio
chanzo kikuu cha mgogoro wa kisiasa ulioigubika Senegal. Wade kama
walivyo viongozi wengine wakongwe wa bara la Afrika, ameazimia
kung'ang'ania madarakani na kuiongoza Senegal hadi mwaka 2022 baada ya
kumalizika vipindi vyake viwili vya kisheria na kwa kuifanyia
marekebisho katiba ya nchi hiyo. Hatua ya Rais Abdullaye Wade wa Senegal mwenye umri wa miaka 85 ya
kutaka kugombea tena katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo ndio
chanzo kikuu cha mgogoro wa kisiasa ulioigubika Senegal. Wade kama
walivyo viongozi wengine wakongwe wa bara la Afrika, ameazimia
kung'ang'ania madarakani na kuiongoza Senegal hadi mwaka 2022 baada ya
kumalizika vipindi vyake viwili vya kisheria na kwa kuifanyia
marekebisho katiba ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment