Saturday, February 18, 2012
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeitisha kikao cha kujadili mgogoro wa Somalia, kikao ambacho kimepangwa kufanyika mjini Cairo Misri hapo kesho. Taarifa zaidi zinasema kuwa, Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limeitisha kikao hicho katika kiwango cha wawakilishi wa kudumu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo chini ya uwenyekiti wa Qatar. Ahmad bin Hilli, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu amesema, kik
ao hicho kitakachohudhuriwa pia na Nabil al-Arabi, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kinatarajiwa kujadili misimamo ya nchi za Kiarabu katika kikao cha kimataifa kuhusiana na Somalia kitakachofanyika Alkhamisi ya wiki hii huko mjini London Uingereza. Bin Hilli amebainisha kwamba, katika mazingira ya hivi sasa nchi za Kiarabu zinatoa kipaumbele juu ya suala la kuisaidia Somalia ili ijiimarishe kiusalama na kuunga mkono serikali ya mpito ya nchi hiyo sambamba na kutoa misaada ya kibinaadamu kwa lengo kuwapunguzia machungu wananchi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika yanayotokana na njaa na ukame.
Posted by
AO Secretarial & Technology Supplies
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment