Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, February 14, 2012

Kenya yawarejeshea Waislamu umiliki wa msikiti mkongwe

Msikiti mkongwe uliojengwa katika karne ya 14 Milaadia unaopatikana katika pwani ya Kenya umerudishwa chini ya umiliki wa Waislamu baada ya mzozo wa muda mrefu kati ya Waislamu na Rais mstaafu Daniel Arap Moi kuhusu mmiliki halali wa ardhi ya msikiti huo.
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameikabidhi kamati ya msikiti huo vyeti 2 vya kumiliki ardhi na kutangaza kuwa serikali ya Nairobi imebatilisha cheti cha kumiliki ardhi kilichoko mikononi mwa Mzee Moi.
Msikiti huo unaojulikana kwa jina la Msikiti wa Congo ambao inasemekana ulijengwa katika karne ya 14 Milaadia, unapatikana kwenye kaunti ya Kwale mjini Diani.
Waislamu wameishukuru serikali kwa kuchukua hatua hiyo walioitaja kuwa ni heshima kubwa kwa matukufu ya dini yao.

No comments: