Jeshi la Mali limekiri kwamba wanamgambo wa Tuareg waliwaua kinyama
baadhi ya wanajeshi wake katika mji wa Aguelhok mwishoni mwa mwezi
Januari.
Jeshi hilo limesema kuwa wanajeshi kadhaa waliuawa kwa kukatwa shingo, wengine wakapigwa risasi vichwani na wengine wakatolewa baadhi ya viungo vyao vya mwili wakati wa vita kati ya wanajeshi na wanamgambo hao. Jeshi limeongeza kuwa raia kadhaa pia waliuawa kwenye hujuma hiyo.
Waasi wa Tuareg wanapigania kujitenga eneo la kaskazini mwa Mali na katika siku za hivi karibuni wamefanikiwa kutekea miji kadhaa ya kistratejia karibu na mpaka wa Mali na Algeria.

No comments:
Post a Comment