Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 9, 2012

Madai ya Sudan Kusini dhidi ya serikali ya Sudan

Serikali ya Sudan Kusini imeituhumu serikali ya Sudan kuwa imevunja makubaliano ya usitishwaji mapigano.
Hayo yamesema hii leo na vikosi vya Sudan Kusini na kuongeza kuwa, vikosi vya Sudan vimevunja makubaliano ya Umoja wa Mataifa kwa kushambulia makazi ya raia wa Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo za Jumatatu na Jumanne. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuzitaka nchi mbili hizo jirani kusitisha mapigano baina yao mara moja na kuongeza kuwa, ikiwa hazitatekeleza azimio hilo la amani basi zitakabiliwa na vikwazo vya kimataifa. Wakati huo huo viongozi wa jimbo la Darfur kusini mwa Sudan wameripoti kutokea mapigano makali baina ya vikosi vya nchi hiyo na kundi la waasi wa Sudan Liberation Army (SLA).

No comments: