Maandamano ya jana ya vijana wanaoipinga serikali ya Guinea Conakry yaligeuka na kuwa vurugu na machafuko baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati. Taarifa zaidi zinasema, maelfu ya vijana wa Guinea Conakry walikuwa wakiandamana dhidi ya serikali na kutoa wito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki wa Bunge katika nchi hiyo. Polisi iliingilia kati maandamano hayo kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji hao hali iliyopelekea kutokea mapigano baina ya pande mbili. Vikosi vya usalama vya nchi hiyo vililazimika kutumia mabomu ya gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao. Makumi ya waandamanaji wamejeruhiwa katika vurugu hizo. Maandamano hayo ya jana yalikwamisha shughuli zote katika mji mkuu Conakry, huku maduka, masoko na hata vituo vya huduma ya petroli vikifungwa kutokana na ghasia zilizozuka baada ya maandamano hayo. Wapinzani wanalalamikia hatua ya Rais Alpha Conde wa nchi hiyo ya kuakhirisha uchaguzi wa Bunge uliopangwa kufanyika mwezi uliopita wa Aprili. Rais Conde ametangaza uchaguzi huo utafanyika Julai 8 mwaka huu na kwamba, umeakhirishwa kutokana na sababu za kiufundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment