Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu imetahadharishwa kwamba karibu watoto milioni moja wanakabiliwa na utapiamlo nchini Yemen huku wengi wao wakiwa hatarini kupoteza maisha. Martin Nesirky amesema kwamba, watoto wa Yemen pia wanakabiliwa na hatari ya mabomu yaliyotengwa ardhini ambayo bado hayajalipuka, yaliyoripotiwa kusababisha vifo vya watoto 13 na kuwajeruhi makumi ya wengine mwaka huu wa 2012.
UN imesema ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo mashirika ya misaada katika nchi hiyo ya Kiarabu yanahitajia msaada wa dola milioni 40 ili kuwasaidia watoto 267,000 wanaokaribia kufa iwapo hawatopata matibabu yanayotakiwa.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umeitaka jamii ya kimataifa iwasaidie mamilioni ya wananchi wa Yemen ambao wanahitajia huduma za afya, maji safi na lishe.

No comments:
Post a Comment