Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail
Showing posts with label ‘Ongezeko la gharama za tiba Moi limebarikiwa na bodi’. Show all posts
Showing posts with label ‘Ongezeko la gharama za tiba Moi limebarikiwa na bodi’. Show all posts

Saturday, May 26, 2012

‘Ongezeko la gharama za tiba Moi limebarikiwa na bodi’


SIKU moja baada ya  gazeti hili kuripoti  habari kuhusu kupanda kwa  gharama za matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili , jijini Dar es Salaam (Moi), uongozi wa taasisi hiyo umetoa ufafanuzi na sababu za kupanda kwa gharama hizo.Akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa Moi, Jumaa Almasi, alisema uamuzi huo umefanywa na Bodi ya Moi.

 “Ni kweli kwamba tumepandisha gharama za matibabu, lakini hatuja kurupuka tu na kufanya maamuzi haya, tulikaa na bodi na kukubaliana,” alisema Almasi.Alisema hata hivyo, gharama hazikupandishwa katika maeneo yote ya tiba na kwamba zimepandishwa katika baadhi ya maeneo.


Almasi alisema sababu ya kupandishwa kwa gharama hizo ni pamoja na  kupanda kwa gharama za vifaa vya kutolea huduma za matibabu.
“Taasisi hii imekuwa ikipokea asilimia 70 ya wagonjwa, wengi wao wakiwa ni  majeruhi kutoka sehemu mbalimbali nchini, kwa hiyo tumefanya hivi hili  kuboresha huduma za matibabu,”alisema Almasi.