Waasi wa Somalia wa al Shabab wameitaka Kenya kuwaachilia huru
Waislamu wote wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi na kutishia kuwa takwa
hilo lisipotekelezwa watawaua mateka wote wa Kenya wanaowashikilia.
Waasi hao wametuma kwenye mtandao wa Tweeter video ya Wakenya wawili
waliowateka nyara katika kaunti ya Wajir mwaka uliopita na kuiambia
serikali ya Kenya kwamba maisha yao yapo hatarini.
Wiki iliyopita waasi wa al Shabab wa Somalia walisema kwamba wamemuua
Denis Allex, jasusi wa Ufaransa waliokuwa wanamshikilia mateka, ili
kulipiza kisasi kutokana na kile walichoeleza kuwa ni uadui wa Ufaransa
kwa Waislamu na mashambulizi yake ya kijeshi nchini Mali.
Kenya inawashikilia watu kadhaa wanaodaiwa kuwa na uhusiano na kundi
la as Shabab na kuhusika katika mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
No comments:
Post a Comment