Huku baadhi ya nchi za Afrika zikiwa zimelazimishwa na Marekani kutofanya biashara ya mafuta na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, nchi nyingine za dunia zinazidi kutafuta njia za kustafidi kwa njia bora zaidi na utajiri huo wa Iran. Jambo hili linaonesha kuweko ubaguzi wa wazi duniani kuhusu vikwazo vya Iran. Hivi sasa Korea Kusini inaendelea kufanya mazungumzo na Iran juu ya njia za kuongeza kiwango cha unuzi wa mafuta hayo huku nchi kadhaa za Magharibi zikifanya mbinu mbalimbali za kukwepa kutekeleza vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran. Siku chache zilizopita, Ayatullahil Udhma Khamenei alisema kuwa, kusamehewa nchi 20 kushiriki katika vikwazo vya mafuta dhidi ya Iran ni katika jitihada za baadhi ya nchi za Magharibi za kukwepa kutekeleza vikwazo hivyo. Wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran nao wameongeza kiwango cha ununuzi wa mafuta hayo. Mwezi uliopita wa Juni, China ilizidisha kiwango cha kunununua mafuta ya Iran kwa asilimia 17 na kufikisha tani milioni 2.6 katika mwezi huo. Hali kama hiyo imeshuhudiwa huku wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran kama vile India, China, Japan na Korea Kusini nao wakisisitiza kuimarisha ununuzi wao wa mafuta ya Iran licha ya vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya kuhusu jambo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment