
Kitengo cha kiintelijensia cha jeshi la Russia GRU kimesema kuwa ndege hiyo ya abiria iliyosababisha vifo vya watu 45 iliangushwa kwa maksudi na Marekani ili kurudisha nyuma jitihada za Moscow za kutawala biashara ya usafiri wa anga katika eneo la Asia na Pasifiki. Ndege hiyo ambayo ni ya kisasa ilikuwa katika safari ya majaribio wakati ilipoanguka Mei 9 nchini Indonesia.
Maafisa wa usalama Russia wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakichunguza harakati za wataalamu wa masuala ya elektroniki wa jeshi la Marekani walio na kituo chao katika uwanja wa ndege wa Jakarta, Indonesia.
No comments:
Post a Comment