Viongozi wa Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi NATO wamekamilisha mkutano wao wa mwaka uliofanyika mjini Chicago Marekani na kukubaliana kwamba wataondoa wanajeshi wa jumuiya hiyo nchini Afghanistan mwishoni mwa mwaka 2014. Viongozi wa NATO wamekubaliana na mpango wa Marekani wa kuondoa taratibu vikosi vya kigeni nchini Afghanistan kuanzia mwishoni mwa 2014 na baada ya hapo jumuiya hiyo itaanza jukumu la kutoa mafunzo na ushauri katika masuala ya kijeshi kwa nchi hiyo. Katika upande mwingine Rais Barack Obama wa Marekani amekutana na Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan pambizoni mwa mkutano huo na kusema kwamba, kampeni za kijeshi za nchi yake nchini Afghanistan na Pakistan zimekuwa zikifanyika kwa lengo la kukabiliana na wale aliowaita kuwa wana misimamo mikali. Obama amedai kuwa, nia ya Washington ni kuona Pakistan yenye demokrasia, mafanikio na uthabiti na kwamba nchi hizo mbili zina adui wa pamoja ambaye ni makundi yaliyofurutu ada yaliyopo nchini humo pamoja na Afghanistan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment