MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO
MAUAJI yanayoambatana na imani za kishirikina yameibuka tena na kuibua hofu ya wakazi wa kijiji cha Myunga wilayani Mbozi mkoani Mbeya na kuwafanya washindwe kufanya kazi za uzalishaji mali kwa amani.
Matukio yaliyozua hofu ni mauaji ya msichana ambaye hajatambuliwa aliyeuawa Aprili 20 mwaka huu na kutupwa katika mto Lwasho ambapo alikutwa na wavuvi ambao walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.
Maiti alibainika kutolewa ulimi, matiti, meno na sehemu za siri hali iliyoamsha hasira za wananchi na wakawataka polisi waliokuwa wamefika eneo la tukio kuondoka na mfanyabiashara Kasandilo Mteka ambaye walimtuhumu kuhusika na mauaji hayo.
Hata baada ya polisi kuondoka na mtuhumiwa huyo wananchi hao waliamua kuvunja nyumba ya mtuhumiwa ambapo walipekua na kuvikuta vitu vinavyodhaniwa kutumika katika kazi hizo za mauaji zikiwemo sindano mbili zilizodaiwa kuwa ni za aina ya BM.
Taarifa za mahojianio kati ya Polisi na mtuhumiwa zimeeleza kuwa mtuhumiwa alimtaja kamanda wa polisi mkoani Tanga kuwa ndiye mwenye vyombo hivyo.
Wananchi hao walimkamata mtuhumiwa mwingine Leonard Simfukwe na kumpiga hadi kumuua ambaye kabla ya mauti aliwataja watu wengine kumi wanaojihusisha na mauaji hayo wakiwemo wengine toka mkoani Rukwa na pia alielekeza kuwa kuna miili mingine mitano imefungwa mawe na kutumbukizwa mtoni ikiwa imenyofolewa baadhi ya viungo ambavyo vinauzwa nchini Zambia.
Katika operesheni hiyo alikamatwa mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Tall Siwiti mkazi wa Miangalua mkoani Rukwa ambaye alinusurika kuuawa kabla ya polisi kumnusuru.
Wananchi walioshuhudia tukio hilo wameseza kuwa watuhumiwa hao hawajaonewa bali mwenendo wao na kazi wanazozifanya ndizo zinawashitaki na kwamba si hao tu bali kundi lote linapaswa kukamatwa na polisi na kama watashindwa basi waowatachukua hatua stahili.
Baadhi ya watuhumiwa waliotajwa wametoroka na kuziacha familia zao wakiwemo wafanyabiashara wa eneo hilo ambapo mmoja wao aliyejulikana kwa jina moja la Simundwe alihamishwa chini ya ulinzi wa polisi.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Myunga Edwin Sikapizye amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba wanasubiri hatua za polisi za uchunguzi ikiwemo utafutaji wa miili hiyo mitano iliyozamishwa mtoni baada ya kuuawa.

No comments:
Post a Comment