Mwakilishi wa Russia katika mazungumzo ya kundi la 5+1 na Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amepinga siasa za Marekani za kuendelea kuiwekea vikwazo Iran.
Sergei Rybakov ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amemwambia mwandishi wa Radio Tehran mjini Baghdad Iraq kwamba, siasa za Marekani za kushadidisha vikwazo dhidi ya Iran hazikubaliki na kwamba Russia inapinga vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Tehran.
Mwakilishi huyo wa Russia katika mazungumzo yanayoendelea mjini Baghdad kati ya Iran na kundi la 5+1 amejibu swali kuhusu je kundi hilo litatambua rasmi haki ya Iran ya kurutubisha urani akisema kwamba: Hakuna mtu anayepinga haki ya Iran ya kurutubisha urani kwani suala la kurutubisha urani ni sehemu ya mambo yanayojadiliwa katika mazungumzo hayo.
Ameongeza kuwa, mbali na masuala ya nyuklia, mazungumzo hayo ya Baghdad yanajadili pia masuala yasiyo ya nyuklia na kumepatikana maafikiano mbalimbali katika masuala hayo.

No comments:
Post a Comment