Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa uingiliaji wa majeshi ya nchi za kigeni katika masuala ya Ghuba ya Uajemi unatishia amani ya eneo hilo la kistratijia.
Ramin Mehmanparast ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ameashiria mazoezi ya kijeshi yanayofanywa na nchi za Kiarabu za kandokando ya Ghuba ya Uajemi na kupelekwa ndege aina ya F22 za Marekani huko Imarati na kusema aina yoyote ya utegemezi wa nchi za eneo hili kwa nchi za kigeni katika masuala ya kijeshi haiwezi kudhamini amani ya eneo hili bali kinyume chake uingiliaji wa majeshi ya kigeni katika Ghuba ya Uajemi unatishia usalama wa eneo hilo. Mehmanparast amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa amani na Ghuba ya Uajemi na nchi za eneo hilo zenyewe. Kuhusu meli iliyokuwa na silaha iliyokamatwa na Lebanon ikielekea Syria, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema baadhi ya nchi zinafanya njama za kukwamisha mpango wa amani wa Kofi Annan kuhusu mgogoro wa Syria na kuchochea vita nchini humo kwa kuyatumia silaha makundi yanayoipinga serikali ya nchi hiyo.
Kuhusu ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza juu ya hali ya haki za binadamu nchini Iran, Mehmanparast amesema inasikitisha kuona viongozi wa serikali ya London wakiingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha kuzungumzia masuala ya haki za binadamu. Ameongeza kuwa ukatili wa polisi ya Uingereza dhidi ya maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika eneo la Tottenham mjini London na mabavu ya polisi dhidi ya harakati ya kupinga ubepari ni ushahidi wa wazi wa hali ya kusikitisha ya haki za binadamu nchini Uingereza na ni bora viongozi wa nchi hiyo washughulikie hali hiyo badala ya kuingilia masuala ya nchi nyingine.

No comments:
Post a Comment