Msemaji wa ikulu ya White House nchini Marekani, Jay Carney amepongeza safari ya Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA hapa nchini na kusema kwamba kuna matumaini ya kutatuliwa kadhia ya nyuklia ya Iran kwa njia za kidiplomasia. Jay Carney amesema safari ya Amano ni hatua nzuri na kwamba muafaka unaotarajiwa kufikiwa kati ya IAEA na Iran karibuni hivi utakuwa na nafasi ya aina yake katika kutatua utata ulioko. Hata hivyo, ikulu ya White House imeendelea kutumia kauli zake za kijuba dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikisema kuwa jamii ya kimataifa itaendeleza mashinikizo dhidi ya Tehran hadi pale kadhia ya nyuklia itakapopatiwa ufumbuzi. Siku ya Jumatatu, Yukiya Amano akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa IAEA aliwasili hapa nchini na kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa serikali ambapo aliitaja ziara yake hapa kuwa ya kihistoria na yenye manufaa mengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment