Umoja wa Mataifa umeonya kuwa baa kali la njaa linahatarisha maisha ya mamilioni ya watu kote magharibi na kati mwa Afrika mwaka huu.
Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya milioni 15 laki sita barani Afrika tayari wameathiriwa vibaya na uhaba wa chakula kutokana na sababu kadhaa zikiwemo ukame, mimea kuharibiwa na wadudu na bei ya juu ya chakula.Mgogoro wa uhaba wa chakula unatazamiwa kuziathiri zaidi nchi za Kiafrika kama vile Chad, Niger, Mali, Mauritania na Burkina Faso.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mwaka huu watoto milioni moja watahitaji msaada wa kuokoa maisha katika eneo la Sahel magharibi mwa Afrika. Aidha Umoja wa Mataifa umesema kunahitajika dola milioni 724 kukabiliana na baa hilo la njaa.
No comments:
Post a Comment