Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 14, 2014

Vikosi vya Misri vyashambulia wanafunzi wa Al Azhar

Vikosi vya usalama vya serikali ya mpito ya Misri inayoungwa mkono na jeshi vimewashambulia wanafunzi waliokuwa wanaandamana katika eneo la bweni katika Chuo Kikuu cha Al Azhar mjini Cairo. Katika patashika hiyo wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu hicho wamejeruhiwa baada ya askari usalama kutumia risasi bandia na gesi ya kutoa machozi katika ghasia hizo.  Tangu jeshi lilipopindua serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Rais Mohamed Mursi mwaka uliopita Chuo Kikuu hicho cha Misri kimekuwa uwanja wa mapambano kati ya askari usalama na wanafunzi.
Itakumbukwa kuwa, Mei 11 mwaka huu korti ya wilaya ya Nasr mjini Cairo iliwahukumu kifungo cha miaka minne jela wanafunzi 36 wa Chuo Kikuu cha Al Azhar huku kila mmoja akipigwa faini ya dola 4,300.

No comments: