Jumuiya ya kieneo ya Mashariki mwa Afrika IGAD imesisitiza
udharura wa kuheshimiwa makubaliano ya usitishaji vita nchini Sudan
Kusini. Seyoum Mesfin mpatanishi wa IGAD katika mgogoro wa Sudan Kusini
amesema, pande mbili zinapaswa kuendeleza mazungumzo na kusitisha vita
sambamba na kujitahidi kutafuta suluhu ya kisiasa katika nchi hiyo ya
mashariki mwa Afrika. Kutokana na mashinikizo ya kimataifa vikosi vya
serikali ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na wanamgambo watiifu kwa
kiongozi wa waasi Riek Machar siku kadhaa zilizopita walilazimika kutia
saini makubaliano ya amani mjini Addis Abbas Ethiopia, lakini bado
vipengee vya makubaliano hayo havijatekelezwa ipasavyo.
Hayo yanaripotiwa huku Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
akitaka kuundwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu waliotenda
jinai dhidi ya binadamu nchini Sudan Kusini.






No comments:
Post a Comment