Umoja wa Mataifa umesema kuwa,
mapigano yameshadidi kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na waasi katika
mkoa wa Kordofan Kusini, na kwamba mahitaji ya misaada ya kibinadamu
katika eneo hilo lenye zaidi ya watu milioni moja yameongezeka. Ofisi ya
Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa,
mapigano hayo yaliyoanza miezi mitatu iliyopita sasa yameshadidi zaidi.
Hayo yanajiri huku jeshi la Sudan
likitangaza kuwa limekomboa mji wa Miri Bara katika mkoa wa Kordofan
Kusini. Khalid Saed msemaji rasmi wa jeshi la Sudan ametangaza kuwa,
vikosi vya serikali jana alasiri viliukomboa mji huo baada ya mapambano
makali na waasi kwenye eneo hilo.







No comments:
Post a Comment