Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 16, 2014

Watu 13 wapoteza maisha kwenye miripuko Nairobi

Habari kutoka Nairobi, Kenya, zinasema kuwa watu takribani 13 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa kufuatia miripuko iliyotokea leo alasiri katika eneo la Gikombaa karibu na kituo kikuu cha mabasi ya mikoani. Mashuhuda wamesema mripuko wa kwanza umetokea ndani ya daladala na mwingine ukatokea muda mfupi baadaye karibu na soko kuu la Gikombaa. Msemaji wa Polisi, Bi Gatiria Mboroki amesema uchunguzi umeanzishwa na kwamba tayari washukiwa wawili wametiwa mbaroni.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta ametoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Rais Kenyatta amesema Kenya inapitia kipindi kigumu katika masuala ya usalama na ametoa mwito kwa Wakenya kushirikiana na vyombo vya usalama katika kukabiliana na vitendo vya ukosefu wa usalama. Kiongozi huyo amekosoa nchi za Magharibi ambazo zimewataka raia wao wasiitembelee Kenya akisema nchi hizo si marafiki wa dhati kwani badala ya kuisaidia nchi yake kukabiliana na ugaidi, zimeamua kutoa onyo kwa raia wao lengo kuu likiwa ni kulemaza sekta ya utalii nchini Kenya.

No comments: