Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 16, 2014

Blatter: Qatar haikufaa kuandaa Kombe la Dunia


Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter, amesema kuwa Qatar haikufaa kupewa fursa ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka mwaka 2022 kutokana na joto kali nchini humo katika msimu wa joto. Blatter amesema FIFA ilishauriwa kuhusiana na hali hiyo lakini kamati husika ikapitisha kwa wingi wa kura kwamba Qatar iandae mashindano hayo. Amesema hilo lilikuwa kosa kubwa ingawa amekumbusha kwamba kila mwanadamu hukosea wakati mmoja au mwingine. Hata hivyo mkuu huyo wa FIFA amekanusha madai kwamba Qatar iliwahonga maafisa wa kamati husika ili kupata nafasi hiyo. Sepp Blatter amesema tuhuma hizo zina malengo ya kisiasa. Mashindano ya kombe la dunia katika mchezo wa soka mwaka huu yatafanyika nchini Brazil, mwaka 2018 yanatarajiwa kufanyika nchini Russia na kisha 2022 yamepangiwa kufanyika nchini Qatar ambapo itakuwa mara ya kwanza kwa nchi ya Mashariki ya Kati kuyaandaa.

No comments: