Serikali ya Uingereza imempatia kinga ya kidiplomasia Waziri wa
Sheria wa utawala wa Kizayuni wa Israel Tzipi Livni, ili kuzuia
asikamatwe atakapoitembelea nchi hiyo kutokana na jinai dhidi ya
binadamu zinazomkabili. Mwaka 2009 mahakama ya Uingereza ilitoa hukumu
ya kukamatwa Livni kutokana na kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la
Israel lililoratibu kuuawa zaidi ya Wapalestina 1,400 katika Ukanda wa
Gaza kati ya Disemba 2008 hadi Januari 2009. Mwaka huo Livni
alilazimika kuvunja safari yake ya kutembelea Uingereza.
Hata hivyo Ofisi ya Jumuiya ya Madola na Masuala ya Nje ya Uingereza
(FCO) imetangaza kuwa, eti imempa 'hadhi ya kutekeleza jukumu maalumu'
Tzipi Livni ambaye anatarajiwa kutembelea London wiki ijayo. Hatua hiyo
imekosolewa na Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu cha Palestina huko
Gaza.







No comments:
Post a Comment