Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 14, 2014

Ja'afari: Israel inawapa mafunzo waasi wa Syria

Syria imeutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa unawaunga mkono wanamgambo wanaopigana dhidi ya serikali ya Rais Bashar la Assad wa nchi hiyo. Bashar Ja'afari Mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Israel inasaidia makundi ya kigaidi katika mapigano hayo na kwamba Tel Aviv imemfadhili, kumpa mafunzo na hifadhi kamanda mpya wa kundi linalojiita Jeshi la Ukombozi wa Syria (FSA).
 Aidha Mwakilishi wa Syria katika moja wa Mataifa ameikosoa Marekani na washirika wake kwa kuingilia masuala ya ndani ya Syria na kuendelea kuuunga mkono makundi ya kitakfiri ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.

 Mwezi Februari kamanda mmoja wa Israel alikiri kwamba jeshi la utawala huo ghasibu linashirikiana na wanamgambo wanaopigana dhidi ya serikali ya Damascus.  Pia ripoti zimeeleza kuwa, mamia ya waasi wanaopigana Syria hupatiwa matibabu katika hospitali za Israel.

No comments: