Rais Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amewataka
Waislamu wanaoishi katika mji mkuu Bangui kutoondoka mjini humo. Rais
huyo wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema hayo
alipokutana na wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za serikali, na
sambamba na kusisitiza udharura wa kulindwa tofauti za kikabila na
kidini katika mji mkuu amewataka Waislamu kutoondoka mjini humo.
Bi. Samba-Panza pia amekiri kuwa hadi sasa mamia ya Waislamu
wamekimbia mji wa Bangui kwa hofu ya machafuko na mapigino na kusema
kuwa, ni lazima serikali iwalinde zaidi Waislamu wanaoishi kwenye mji
huo.
Kwa miezi kadhaa sasa Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
wamekuwa wakishambuliwa na genge la Wakristo la Anti Balaka, huku nyumba
zao na misikiti ikibomolewa.
Hayo yanajiri huku Marekani ikimuwekea vikwazo rais wa zamani wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize pamoja na watu wengine wanne
waliohusika katika machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini
humo.







No comments:
Post a Comment