Mkutano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa
Nishati ya Atomiki (IAEA) umemalizika hapa mjini Tehran huku pande mbili
hizo zikielezea kufurahishwa na anga ya kirafiki ya mkutano huo. Ujumbe
wa IAEA ulikutana na maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Iran jana
Jumanne na kufanya mazungumzo ya kina kuhusiana na miradi ya nyuklia ya
hapa nchini yenye malengo ya amani. Ingawa taarifa rasmi ya mkutano huo
haijatolewa lakini baadhi ya wajumbe na wanadiplomasia waliohudhuria
kikao hicho wamesema majadiliano yalikuwa ya kina na anga ya kirafiki
ilitanda katika kipindi chote cha mkutano.
IAEA na Iran zimekubaliana
kuendeleza mazungumzo katika siku za usoni ili kuongeza zaidi kasi ya
ushirikiano wa pande mbili. Mkutano huo umefanyika siku chache kabla ya
kutolewa ripoti ya wakala huo wiki hii. Ripoti hiyo itajadiliwa baadaye
mwezi ujao kwenye mkutano wa Bodi ya Magavana wa IAEA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment