Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 21, 2014

AU: Pande za Sudan ziitikie wito wa mazungumzo

Umoja wa Afrika umezitaka pande zote za Sudan kuitikia wito wa mazungumzo ya kitaifa. Nkosazana Dlamin Zuma Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa ya Sudan kwa ajili ya mutakbali wa nchi hiyo na kuzitaka pande zote za nchi hiyo kutopoteza fursa ya mazungumzo hayo. Katika taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika, Zuma amesema AU inatiwa wasiwasi na mabadiliko yanayojiri nchini Sudan kwani mabadiliko hayo yanaweza kuwa na taathira hasi kwa mwenendo wa mazungumzo ya kitaifa.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amesisitiza kuwa AU inashikamana na ahadi yake ya kuisaidia Sudan kufanikisha mazungumzo hayo ya kitaifa.
Mwezi Januari Rais Omar al Bashir wa Sudan alitoa pendekezo la kufanyika mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa na makundi na vyama vya upinzani na pia harakati za waasi kama njia ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo.

No comments: