Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amesema Shirika Kuu la Kijasusi la
Marekani CIA linaficha maelezo muhimu kuhusu hatima ya ndege ya Malaysia
iliyotoweka. Katika taarifa aliyochapisha katika weblogu yake siku ya
Jumapili, Mahathir Mohammad amesema CIA na shirika la utengenezaji
ndege la Marekani, Boeing, kwa pamoja zinaficha maelezo kuhusu ndege
iliyotoweka. Aidha amesema ni jambo la kushangaza kuona vyombo vikubwa
vya habari duniani havifuatlii kwa kina kadhia ya ndege hiyo ya
Malaysia.
Mahathir amesema yamkini CIA iliongoza ndege hiyo kwa mbali na
kuiweka katika mfumo wa kujiendesha yenyewe kisha ikatua eneo la siri
na alama zake za Malaysian Airlines kuondolewa. Ndege hiyo ya Shirika la
Ndege la Malaysia iliyotoweka tarehe 8 mwezi wa Machi mwaka huu ikiwa
na mamia ya abiria ilipokuwa inaelekea Beijing, China kutoka Kuala
Lumpur Malaysia. Pamoja na kuwa nchi kadhaa zinashirikiana katika juhudi
za kuitafuta ndege hiyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa lakini bado
hakuna athari zozote za ndege hiyo ya kisasa aina ya Boeing 777-200ER
iliyotengenezwa Marekani. Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak naye pia
alinukuliwa akisema ndege ya abiria ya nchi hiyo iliyotoweka ilipotoshwa
mkondo wake kwa makusudi na kuendelea kuruka angani masaa kadhaa hata
baada ya kutoweka kwenye rada.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment