Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 16, 2014

Zaidi ya 160 wamefariki kwa virusi vya MERS Saudia

Maafisa wa Afya wa Saudi Arabia wametangaza kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na virusi vinavyoshambulia mfumo wa kupumua vya coronavirus au MERS imefikia 160, ikiwa ni baada ya kufariki dunia watu watatu hapo jana.  Wizara ya Afya ya Saudia imesema kuwa, vifo hivyo vimetokea katika mji mkuu Riyadh, na miji ya magharibi ya Jeddah na Madina. 

Ripoti zinaonesha kuwa, tangu virusi hivyo vilipoguduliwa nchini humo hadi sasa watu karibu 500 wameambukizwa ugonjwa huo. MERS ni virusi vya kundi la Coronavirus vinavyojumuisha vimelea vinavyosababisha mafua au matatizo katika mfumo wa kupumua. Virusi hivyo husababisha maambukizi kwenye mapafu, ambapo mgonjwa hukohoa, hushindwa kupumua na husumbuliwa na homa.

No comments: