Shirika la kimataifa la
kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani ukiukwaji wa
haki za binadamu nchini Bahrain sambamba na kukosoa mwendo wa kobe wa
serikali katika kufanya mageuzi katika idara ya mahakama. Shirika hilo
limesema kwenye ripoti yake kwamba, utawala wa Aal Khalifa umeshindwa
kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya maafisa wake waliotenda jinai
dhidi ya binadamu; jambo linalokiuka sheria za kimataifa. Ripoti hiyo ya
Amnesty International inafuatia uchunguzi wa kina wa shirika hilo
wakati wa ziara yake nchini Bahrain.
Maafisa wa AI walikuwa Bahrain kati
ya Mei 3 hadi 9 ambapo walikutana na watu mbalimbali wakiwemo wafungwa
wa kawaida na wale wa kisiasa.
Taarifa ya Amnesty
International imeitaka serikali ya Manama kuchukua hatua za dharura
kulinda uhuru wa kujieleza na kukutana wa raia wa nchi hiyo.







No comments:
Post a Comment