Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 10, 2012

Zimbabwe yalaani uamuzi wa Afrika Kusini wa kuendesha kesi za kipindi cha Mugabe

Waziri wa Mahakama wa Zimbabwe amelaani uamuzi wa Mahakama ya Afrika Kusini wa kusema kwamba inaweza kuruhusu kusikiliza nchini humo kesi zinazohusu mateso yanayodaiwa kufanywa chini ya utawala wa Rais Robert Mugabe.
Patrick Chinamasa amesema kwamba, uamuzi huo unaupa jina baya mfumo wa sheria wa Afrika Kusini na ingawa hakuna maelezo ya wazi yaliyotolewa lakini Pretoria inapaswa kuweka wazi jinai zilizotendeka kabla ya kuchukua hatua hiyo.
Mateso hayo ni yake yanayodaiwa kufanywa na maafisa wa Zimbambwe ya kuwatesa wanaharakati kadhaa wa kisiasa baada ya kuvamiwa makao makuu ya chama cha MDC mwaka 2007. Hatua hiyo ya Afrika Kusini imepongezwa na chama cha MDC pamoja kiongozi wake Morgan Tsvangirai ambaye ni Waziri Mkuu wa Zimbabwe katika serikali ya umoja wa kitaifa na chama cha Mugabe.
 

No comments: