Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

Umoja wa Ulaya wataka kuanzishwa mahakama maalumu kwa ajili ya maharamia

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, unataka kuanzishwe mahakama maalumu ya kuwashtaki na kuwahukumu maharamia wa Somalia sambamba na kushadidishwa vita dhidi ya maharamia hao. Wabunge  wa Bunge la Umoja wa Ulaya wamepasisha kwa wingi wa kura uamuzi wa kutaka kuanzishwa mahakama maalumu ya kushughulikia kesi za maharamia wa Somalia. Taarifa ya Bunge la Umoja wa Ulaya iliyotolewa huko Brussels Ubelgiji imebainisha kwamba, haiwezekani kupambana na maharamia wa Somalia katika pwani ya mashariki mwa Afrika kwa kutumia njia za kijeshi pekee. Aidha Bunge la Umoja wa Ulaya limeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za maana katika kupambana na maharamia wa Somalia ambao wamehatarisha usalama katika pwani ya mashariki mwa Afrika.

No comments: