Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

39 WAHOJIWA KUHUSU MAUAJI YA ST. AUGUSTINE - MWANZA

POLISI mkoani Mwanza inawashikilia watu 39 waliokamatwa katika msako uliofanyika maeneo ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine(Saut) kwa mahojiano juu ya mauaji ya utata yaliyotokea katika hosteli za wanafunzi wa chuo hicho.

Mauaji hayo yalitokea kati ya Machi 9 hadi Mei 4, mwaka huu ambapo watu sita akiwemo mwanafunzi wa Saut waliuawa na watu wasiojulikana na wengine miili yao kuchomwa moto. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Deusdedit Nsimeki alisema msako huo ulianza mwishoni mwa wiki iliyopita na kwamba watuhumiwa hao walifanyiwa mahijiano ili kuwabaini walioshiriki kwenye vitendo vya mauaji.

No comments: