Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

Sudan yakanusha madai ya Sudan Kusini ya kushambuliwa ardhi yake

Serikali ya Sudan imekanusha madai ya jirani yake Sudan Kusini kwamba, vikosi vya Khartoum vimeshambulia maeneo ya Juba. As-Sawarmi Khalid, msemaji wa jeshi la Sudan amesema kwamba, madai ya viongozi wa Juba kwamba, jeshi la Khartoum limeshambulia kwa mabomu baadhi ya maeneo ya nchi hiyo hayana ukweli wowote. Amesema, Khartoum inafungamana kikamilifu na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kuhitimishwa uhasama baina ya nchi hizo mbili. Msemaji wa jeshi la Sudan ameongeza kwamba, tangu Sudan Kusini ijitangazie uhuru, Khartoum haijawahi kufanya shambulio hata moja dhidi ya nchi hiyo; ilhali Juba imefanya uvamizi mara kadhaa dhidi Khartoum. Ameashiria uvamizi uliofanywa na vikosi vya Juba huko Heglig, Abyei na Kordofani Kusini na kubainisha kwamba, huu ni ushahidi wa wazi kwamba, Juba ndio ambayo imekuwa ikianzisha uchokozi.

No comments: