Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

FAO: Tunakabiliwa na upungufu wa bajeti ya misaada Sahel na Pembe ya Afrika

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha kuhusiana na upungufu mkubwa wa bajeti linaokabiliwa nao katika harakati zake za kwenye maeneo ya Sahel na Pembe ya Afrika. Jose Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO amesema katika warsha ya kiuchumi huko Madrid Uhispania kwamba, licha ya kuweko hatua zilizochukuliwa kwa ajili ya kudhamini usalama wa chakula lakini bado kungali kuna matatizo ambapo shirika hilo linakabiliwa na upungufu wa bajeti katika kutekeleza mipango yake. Jose Graziano da Silva, ameongeza kwamba, kuna baadhi ya maeneo ulimwenguni ambayo yanakabiliwa na hali mbaya ya chakula kama eneo la Sahel na Pembe ya Afrika. Aidha amekiri kwamba, kila kati ya watu saba mmoja anakabiliwa na lishe duni ulimwenguni. Amesema, tishio la njaa ni kubwa na kwamba, FAO peke yake au serikali ya nchi moja haiwezi kukabiliana nalo.

No comments: