Mkankanyiko huu nimeukuta mtandao wa Wanabidii.
Hoja hii hapa;
Nimekuwa sielewi sifa ya kuwa mbunge kamili ni mpaka uwe umeapishwa na Spika bungeni au inakuwaje? Maana nimeona Mh Rais kawateuwa wabunge na mwingine leo mchana,ila tayari amewateuwa tena kuwa Mawaziri. Pengine sielewi Katiba inasemaje ndo maana nimeomba mnipatie mwongozo..

Kimantiki lazima mtu anabaki Mbunge Mteule hadi hapo anapoapishwa ndipo anakuwa Mbunge. Hivyo hivyo mtu atabaki Waziri Mteule hadi hapo anapoapishwa kuwa Waziri na mtu awezi kuapishwa kuwa Waziri kabala hajaapishwa kuwa Mbunge. Hiyo ni kimantiki lakini bado wanasheria ndani humu watusaidie vifungu vya sheria vinasemaje. Nitashangaa kama sheria itakuwa kinyume cha mantiki!!!







No comments:
Post a Comment