![]() |
| Ban Ki Moon - Katibu mkuu wa UN |
Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa kukabiliana vilivyo na kwa usawa na suala la ugaidi duniani.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama cha kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ugaidi, Ban ametaka kufanywe jitihada za pamoja katika uwanja huo na kusema kuwa, mapambano dhidi ya ugaidi yanapaswa kufanya kwa kushirikishwa mataifa yote ili kupunguza tishio dhidi ya amani na usalama duniani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aidha amesema, ugaidi ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa watu wote duniani na kuongeza kuwa, ijapokuwa jitihada za kupamba na ugaidi zinafanyika lakini mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Afghanistan, Iraq, Nigeria na Yemen yanaonesha kuwa suala hilo bado ni tishio.

No comments:
Post a Comment